Storm FM

TANROADS Geita yatimiza ahadi Nyantorotoro

18 May 2024, 12:21 pm

Gari ikipita katika barabara iliyofanyiwa marekebisho. Picha na Kale Chongela

Ikiwa ni muda wa wiki moja sasa tangu wananchi wa Nyantorotoro A kuamua kufunga barabara kuu ili kushinikiza matengenezo ya barabara hiyo hatimaye TANROADS wafanya marekebisho.

Na: Kale Chongela – Geita

Wakazi wa mtaa wa Nyantorontoro A ulipo kata ya Nyankumbu halmashauri ya mji wa Geita wameushukuru uongozi wa TANROADS mkoa wa Geita kwa kutimiza ahadi ya kuweka alama za barabarani.

Baadhi ya wananchi wa eneo hilo wamesema kufuatia changamoto ya baadhi ya madereva kuendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi iliwapa wakati mgumu juu ya hatma yao hususani watoto wanapotumia barabara hiyo.

Sauti ya wananchi

Meneja wa TANROADS mkoa wa Geita Mhandisi Ezra Magogo amesema kuwa uwekaji wa alama hizo utawaongoza madereva kupunguza mwendo kasi na kwamba ni jukumu lao kuhakikisha kila barabara ina alama ili kupunguza ajali za barabarani.

Sauti ya meneja TANROADS