Storm FM

Mashabiki Geita waviaminia vilabu vya Tanzania CAF

28 July 2023, 9:15 am

Mashabiki wa soka Geita. Picha na Zubeda Handrish

Kwa mara nyingine tena vilabu vya Tanzania vinakwenda kuiwakilisha nchi katika michuano ya CAF kwa upande wa Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho, Je watafika mbali?

Na Zubeda Handrish- Geita

Droo ya hatua mbili za awali za michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao, imechezeshwa Julai 25, 2023 huko Cairo, Misri huku vilabu mbalimbali vikibaini wapinzani wao kwenye hatua walizopangiwa.

Sauti ya shabiki wa soka Geita

Vilabu vya Tanzania kwa upande wa Klabu Bingwa Yanga SC itaanzia hatua ya awali (first preliminary round) imepangwa dhidi ya klabu ya AS Djibouti Telecom ya Nchini Djibouti kwenye hatua hiyo, huku Simba SC ambayo itaanzia raundi ya pili ya mchujo ya Ligi ya Mabingwa Afrika itachuana na mmoja kati ya Mabingwa wa Zambia Power Dynamos au Mabingwa wa Namibia, Africans Stars FC.

Moja ya shabiki wa soka akitoa maoni yake. Picha na Zubeda Handrish

Kombe la Shirikisho Klabu ya Singida Fontaine Gate FC itachuana na vigogo wa visiwani Zanzibar JKU SC na Azam FC itachuana na Bahir Dar Kenema ya Ethiopia, kufuatia droo hii mashabiki wa soka Geita wamefunguka juu ya hatma ya vilabu hivi.

Sauti ya shabiki wa soka Geita