Storm FM

Vyoo, visima na nyumba vyazingirwa na maji Ibolelo, Geita

6 December 2023, 8:22 am

Hali ilivyo katika mtaa wa Ibolelo mjini Geita. Picha na Evance Mlyakado

Ni moja ya eneo lililopo mtaa wa Ibolelo, kata ya Nyankumbu mjini Geita ambalo limeathirika na mvua, Je wananchi wanaishi vipi katika mazingira haya?.

Na Evance Mlyakado- Geita

Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Geita zimeendelea kuleta changamoto kwa wakazi wa mjini Geita baada ya nyumba kadhaa kuzingirwa na maji huku baadhi ya vyoo na visima vikifurika maji katika mtaa wa Ibolelo maarufu kwa jina la Mwabasabi uliopo kata ya Nyankumbu katika Halmashauri ya Mji wa Geita.

Hali ilivyo katika mtaa wa Ibolelo mjini Geita. Picha na Evance Mlyakado

Wakizungumza na Storm FM wananchi hao wamesema mvua iliyonyesha jana Disemba 06, 2023 majira ya asubuhi ndio imesababisha maji kujaa katika makazi yao hali iliyowapelekea wananchi hao kushindwa kuendelea na shughuli zao za kila siku huku wakihofia usalama wa mali na Afya zao.

Wananchi wa mtaa wa Iboleo uliopo kata ya Nyankumbu, halmashauri ya mji wa Geita wakizungumzia kero wanayoipata baada ya maji hayo kuzingira makazi yao.