Storm FM

Mbwa tishio Shilabela.

17 September 2021, 5:37 pm

Na Zubeda Handrish:

Katika hali isiyokuwa ya kawaida watu 8 wameng’atwa na mbwa katika mtaa wa Shilabela mjini Geita ikielezwa kuwa ni mbwa wenye kichaa.

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa mtaa huo Bw. Fredrick Masalu baada ya wahanga kufika ofisini kwake ili kuweza kupata kibali cha matibabu.