Storm FM
Storm FM
18 September 2026, 3:57 pm

Mkuu wa mkoa wa Geita katika mkutano wa hadhara. Picha na Mrisho Sadick
Gari la kifahari aina ya Toyota Land Cruiser V8, linalotumiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, litumike kubebea wagonjwa katika Kituo cha Afya Muganza.
Na: Mrisho Sadick
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Alexander Mnyeti, ameamuru gari la kifahari aina ya Toyota Land Cruiser V8, linalotumiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, litumike kubebea wagonjwa katika Kituo cha Afya Muganza.
Mnyeti alitoa agizo hilo karibuni katika mkutano wa hadhara uliofanyika Soko la Dagaa Kasenda, Kijiji cha Nyabugera, baada ya wananchi kulalamikia kukosekana kwa gari la wagonjwa katika kituo hicho kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Malalamiko hayo yaliwasilishwa na Mbunge wa Chato Kaskazini, Cornel Magembe, aliyesema gari la wagonjwa la kituo hicho limekuwa nje ya huduma kwa zaidi ya mwezi mmoja kutokana na kukosa matairi.
Sauti ya mbunge wa Chato Kaskazini
Akikemea hali hiyo, Mnyeti amesema haikubaliki maisha ya wananchi kuhatarishwa kwa sababu ya ukosefu wa matairi, akisisitiza kuwa suala hilo lingeweza kutatuliwa mapema na uongozi wa Halmashauri.
Sauti ya mkuu wa mkoa wa Geita