Storm FM
Storm FM
9 September 2026, 3:54 pm

Baada ya Geita Gold FC kumalizana na Simba SC sasa silaha zao wamezihamishia kwa wananchi Yanga ambapo mchezo huo utapigwa hivi karibuni.
Na Mrisho Sadick:
Klabu ya Geita Gold FC imeendelea na maandalizi kuelekea mchezo wake dhidi ya Yanga SC utakaochezwa Septemba 15 jijini Dar es Salaam ikiwa na rekodi ya kushinda michezo miwili kati ya mitano iliyocheza katika Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.
Msemaji wa Geita Gold FC Samweli Dida akiwa katika Geita Gold Media Day amesema mchezo huo hautakuwa mwepesi kutokana na ubora wa wapinzani wao hivyo klabu imefanya maandalizi ya kina kuhakikisha timu inaingia uwanjani ikiwa tayari kwa ushindani na kupata ushindi.

Naye Nahodha wa Geita Gold FC Yusuph Mhilu pamoja na wachezaji wengine wamewataka vijana wanaojitafuta kwenye soka kutokata tamaa wanapokutana na changamoto bali waendelee kufanya mazoezi, kuwa na nidhamu na kupambana kwa bidii ili kutimiza ndoto zao.