Storm FM

Akamatwa ugoni kwa mtego wa siri Bukombe

4 June 2025, 6:33 pm

Mtuhumiwa wa ugoni akiwa chini ya ulinzi ofisi ya kitongoji. Picha na Mwandishi wetu

Msemo wa mke wa mtu sumu umedhihirika kwa kijana Kake baada ya kuonja joto la jiwe kwa kudaiwa kuwa katika mahusiano na mke wa mtu.

Na Mwandishi Wetu Bukombe:

Kijana mmoja mkazi wa kitongoji cha Bukingwamizi Kijiji cha Nalusunguti Kata ya Busonzo wilayani Bukombe Mkoani Geita amekamatwa ugoni baada ya mume wa mwanamke huyo kuweka mtego nakufanikiwa kumnasa.

Akizungumza katika ofisi ya Kitongoji hicho Juni 02,2025 Edga Sotel mume wa mwanamke huyo amesema baada ya kuhisi kuwa mke wake anamsaliti kimapenzi na mwanaume mwingine ambae ni ndugu yake yani mtoto wa kaka yake ameoa nyumbani kwa kijana huyo ambae anajihusisha na mapenzi na mke wake ndipo alipoamua kutumia akili ya ziada kwa kuweka mtego wa siri wa rekodi kwenye simu ya mke wake huku mwanamke huyo akiomba msamaha kwa kitendo hicho.

Sauti ya Mume na Mke

Akiwa chini ya ulinzi katika ofisi ya kitongoji hicho kijana huyo ambae ametambulika kwa jina la Mengineyo Kake ameanza kwa kutambua kuwa mke wa mtu ni sumu huku akichutama kuomba msamaha kwa familia ya Sotel , viongozi wa serikali ya kijiji na wakazi wa kitongoji hicho kwa kitendo hicho.

Sauti ya Mtuhumiwa

Viongozi wa jeshi la jadi sungusungu katika eneo hilo waliofanikisha kumnasa kijana huyo Bupilipili Isack na Jumanne Matulanya wamesikitishwa na kitendo hicho huku wakiwataka vijana katika kijiji hicho kuacha tabia hiyo kwakuwa ni hatari kwa usalama wao.

Sauti ya viongozi wa Sungusungu

Mwenyekiti wa kitongoji hicho Philipo Mashinga amekiri kumshilikia kijana huyo huku akimpongeza mwanaume huyo kwakutochukua sheria mkoani nakuamua kufika kwa uongozi nakwamba mtuhumiwa amepigwa faini ya shilingi laki mbili na elfu 70 nakutakiwa kutotenda kosa kama hilo tena katika kitongoji hicho.