Storm FM

Wanawake Nyankumbu waondokana na adha ya kujifungulia njiani

13 April 2024, 1:55 pm

Baadhi ya wanawake kutoka kata ya Nyankumbu waliohudhuria kupata huduma katika kituo cha Afya Nyankumbu. Picha na Mrisho Sadick

Changamoto ya wanawake kujifungulia njiani imekuwa ikiripotiwa kutoka katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu huku sababu mbalimbali ikiwemo Umbali, uchumi na miundombinu duni katika baadhi ya maeneo ya kutolea huduma za afya zikihusishwa kupelekea hali hiyo kutokea.

Na Mrisho Sadick – Geita

Idadi ya wanawake wanaojifungulia njiani katika Kata ya Nyankumbu Halmashauri ya Mji wa Geita Mkoani Geita imepungua kutokana na serikali kuimarisha huduma za afya kwenye Kituo cha Afya Cha Kata hiyo.

Muonekano wa kituo cha Afya cha kata ya Nyankumbu halimashauri ya mji wa Geita. Picha na Mrisho Sadick

Wanawake waliofika kwenye kituo Cha Afya Nyankumbu kujifungua wamesema kuimarishwa kwa huduma katika eneo hilo imekuwa chachu kwa wanawake wengi kujitokeza kwa wingi.

Sauti za wanawake waliofika kupata huduma kituo cha Afya Nyankumbu

Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho Dkt Irene Temba amesema Idadi ya wanawake wanaojifungulia njiani imepungua kutoka 80 hadi 4 kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Sauti ya Mganga Mfawidhi Kituo Cha Afya Nyankumbu.

Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa Magambo Magambo na Katibu wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Geita Rehema Mtawala wamesema  mbali na Jumuiya hiyo kufanya  usafi , nakutoa Msaada kwa wagonjwa wameipongeza serikali kwa kuimarisha huduma kwenye kituo hicho.

Sauti za viongozi wa jumuiya ya wazazi Geita
Baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya wazazi Geita. Picha Mrisho Sadick