Storm FM

Watoto wawili wafariki dunia kwa kuzama bwawani.

6 January 2023, 9:03 am

Na Kale Chongela:

Watoto wawili,  Jebra Michael mwenye umri wa miaka (3) na  Mariam Ndarahwa mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu wakazi wa Mtaa wa Nyantorotoro B, Halmashauri ya mji wa Geita wamefariki Dunia kwa kuzama Bwawani wakati wakiwafuata wazazi wao walipokuwa wakienda shambani.

Wakizungumzia tukio hilo Wakazi wa Mtaa huo akiwemo mwenyekiti wa serikali ya Mtaa huo wamesema Watoto hao wamezama katika Bwawa hilo toka jana na miili yao wameikuta inaelea juu ya maji siku ya leo katika bwawa ambalo lipo katika barabara ya kwenda shambani kwa wazazi wa watoto hao.

Kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoani Geita, Staff Sajenti Emmanuel Ndoshi akiwa eneo la tukio amezitaka serikali za mitaa, vitongoji na vijiji Mkoani kuhakikisha wanafanya oparesheni ya kukagua maeneo hatarishi nakuyawekea alama ili kuepukana na ajali kama hizo.