Storm FM

Mwanaume (32) wilayani Chato ajinyonga hadi kufa

9 April 2021, 12:16 pm

Na Mrisho Sadick:

Mtu mmoja mwenye umri wa miaka (32)  mkazi wa kijiji cha Izumangabo kata ya Bwanga wilayani chato mkoani Geita amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kikoi cha mke wake huku chanzo cha tukio hilo kikiwa bado hakijafahamika.

Tukio hilo limetokea April 8, 2021 majira ya saa saba mchana baada ya Mke wake kwenda sokoni na aliporudi alikumkuta mume wake akiwa amejinyonga juu ya dali, ndipo alipokwenda kwa majirani kutafuta msaada wa kumuondoa katika eneo hilo.

Mke wa Marehemu

Ndugu wa marehemu huyo wamesikitishwa na tukio hilo huku wakisema kuwa kabla ya kifo chake alikuwa akiugua na alipelekwa katika kituo cha afya cha bwanga kupatiwa matibabu kisha kuruhusiwa kurudi nyumbani nakufanya tukio hilo.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Izumangabo Bw Innocent Marko amemtaja aliefariki dunia kuwa ni Seleman Shaban mwenye umri wa miaka (32)  mkazi wa kijiji hicho, huku chanzo cha tukio hilo kikiwa bado hakijafahamika na marehemu ameacha watoto wanne na mwanamke mmoja.