Storm FM

Manara ashangazwa ligi ya Misungwi Cup Ludete Katoro

16 August 2026, 5:09 pm

Msemaji wa Timu za Taifa Tanzania Haji Manara akiwa katika michuano ya Misungwi Cup. Picha na Mrisho Sadick

Manara ashangazwa na umati mkubwa wa mashabiki katika fainali ya misungwi Cup Kata ya Ludete mamlaka ya mji wa Katoro wilayani Geita.

Na Mrisho Sadick:

Msemaji wa Timu za Taifa Tanzania Haji Manara amezitaka mamlaka za Serikali mkoani Geita kujenga uwanja wa michezo wa kisasa katika mji mdogo wa Katoro akisema eneo hilo lina mwamko mkubwa wa michezo na lina uwezo wa kuzalisha vipaji.

Manara ametoa wito huo akiwa mgeni maalumu katika fainali ya michuano ya Misungwi Cup iliyofanyika katika Kata ya Ludete, mji mdogo wa Katoro wilayani Geita, ambapo maelfu ya wananchi walijitokeza kushuhudia fainali hiyo.

Maelfu ya wananchi wakiwa kwenye fainali ya michuano ya Misungwi Cup Kata ya Ludete Katoro Geita. Picha na Mrisho Sadick

Katika mchezo huo California FC iliibuka na ushindi wa mabao 4–1 dhidi ya Katoro Centre na kujinyakulia zawadi ya shilingi milioni 5 za Kitanzania.

Akizungumza katika fainali hiyo Manara amesema uwanja wa kisasa utasaidia kukuza vipaji na kuongeza hamasa ya michezo katika eneo hilo huku Mkuu wa Wilaya ya Geita kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa akiahidi kulifanyia kazi suala hilo.

Msemaji wa Timu za Taifa Tanzania Haji Manara akizungumza katika fainali ya Misungwi Cup. Picha na Mrisho Sadick

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Ludete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Jumanne Misungwi amesema michuano hiyo itaendelea kufanyika kwa lengo la kuibua na kukuza vipaji vya vijana.

Ripoti kamili ya Stori hii na Mrisho Sadick