Storm FM
Storm FM
3 August 2026, 1:15 pm

Tamasha hilo litafanyika ikiwa ni sehemu ya utambulisho wa Uwanja mpya wa kisasa wa Bukombe, ambao utatumika na Geita Gold FC katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2026/2027.
Na Mrisho Sadick:
Waandaaji wa Tamasha la Joto la Ligi Kuu linalotarajiwa kufanyika Agosti 4, 2026 Wilayani Bukombe, mkoani Geita wametangaza rasmi viingilio vya tukio hilo litakalomshirikisha Klabu ya Yanga SC pamoja na burudani mbalimbali.
Kwa mujibu wa waandaaji kiingilio cha kawaida ni shilingi 10,000 daraja la pili shilingi 20,000 VIP B shilingi 50,000 VIP A shilingi 100,000 huku VVIP ikiwa ni shilingi 150,000.
Tiketi zitapatikana kwa njia ya mtandao pamoja na mauzo ya kawaida katika vituo mbalimbali vilivyotengwa. Maeneo ya mauzo ni Katoro, Runzewe, Masumbwe, Mgodi wa Msasa na Kahama.
Kwa upande wa Ushirombo, tiketi zitapatikana katika vituo vya DF Hotel, The One Barbershop, Kitambaa OG na Kilimahewa karibu na Uwanja huo wa Bukombe.