Storm FM

Changamoto za malighafi zawakabili wahunzi Ikulwa

10 September 2026, 6:37 pm

Picha ya vyuma vikiwa vinachemshwa kwenye moto kwaajili ya utengenezaji wa vifaa. Picha na Kale Chongela

Uongozi wa mtaa unatambua mchango wa kundi hilo na utaendelea kulitambua na kulithamini kutokana na shughuli wanazofanya katika kujipatia kipato.

Na: Kale Chongela

Wajasiriamali wanaojihusisha na shughuli za uchakataji wa vyuma waliopo Mtaa wa Ikulwa Kata ya Ihanamilo Manispaa ya Geita wameeleza kuwa shughuli hiyo imekuwa chanzo muhimu cha kipato kinachowasaidia kukidhi mahitaji ya familia zao.

Wakizungumza na Storm baadhi ya wajasirialiamali hao wamesema kupitia kazi hiyo wameweza kujipatia kipato huku wakibainisha kuwa licha ya jitihada wanazojifanya zipo changamoto ambazo zinawakabili ikiwemo upatikanaji wa malighafi za kutengeza mikuki,Moko na mishale.

Sauti ya baadhi ya wajasirialiamali

Wahunzi wakiwa wanagonga vyuma kutengeneza mikuki, moko na mishale

Akizungumza Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Ikulwa kwa niaba ya Mwenyekiti wa Mtaa huo Bi Rehema Shija amesema uongozi wa mtaa unatambua mchango wa kundi hilo na utaendelea kulitambua na kulithamini kutokana na shughuli wanazofanya katika kujipatia kipato.

Sauti ya mjumbe wa serikali ya mtaa wa Ikulwa