Storm FM

Geita kujenga vituo vya polisi kila kata kukabiliana na uhalifu

31 July 2023, 5:40 pm

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Geita wakiwa katika kikao cha baraza. Picha na Mrisho Sadick

Bajeti zinazopitishwa na halmashauri ya wilaya ya Geita na Mji wa Geita zimetakiwa kuzingatia vipaumbele vya ujenzi wa vituo vya polisi kila kata wilayani humo ili kukabiliana na vitendo vya uvunjifu wa amani.

Na Mrisho Sadick:

Wilaya ya Geita imeweka mkakati wa kukabiliana na matukio ya uvunjifu wa amani ikiwemo vitendo vya uhalifu kwa kuimarisha ulinzi shirikishi pamoja na kujenga vituo vya polisi kila Kata.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Geita wakati akitoa taarifa ya ulinzi na usalama wilaya ya Geita.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Geita
Mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe akizungumza katika baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Geita. Picha na Mrisho Sadick

Baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo wamepongeza hatua hiyo kuwa itasaidia kupunguza matukio ya uhalifu katika halmashauri hiyo.

Sauti ya Madiwani

Katibu wa chama cha ACT Wazalendo mkoani Geita Ikolongo Otto amesema mkakati huo utakuwa na tija iwapo utafanyiwa kazi ipasavyo.

Sauti ya Mwenyekiti wa ACT Wazalendo