Storm FM

Viongozi wa dini waonya serikali kulaumiwa kwa majanga ya asili

16 April 2024, 9:05 pm

Viongozi wakuu wa makanisa ya PCMA Tanzania wakiwa katika kongamano la kuliombea taifa na viongozi wake. Picha na Nickolaus Lyankando

Kuendelea kutokea kwa majanga ya asili hapa nchini baadhi ya wananchi wameanza kuinyoshea kidole serikali huku baadhi ya viongozi wa dini wakionya.

Na Nickolaus Lyankando – Geita

Watanzania wametakiwa kuacha tabia ya kuilaumu serikali kutokana na majanga ya asili ambayo yanatokea hususani mafuriko nabadala yake  waungane kwa pamoja  kuliombea taifa ili kuepuka majanga hayo.

Kauli hiyo imetolewa na Askof  wa makanisa ya Presbterian,central mission of Africa PCMA nchini Tanzania  Bishop Mondeha Kabeho katika kongamano la siku nne la kuliombea taifa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan lililofanyika katika Kanisa la Mlima wa Moto katoro Mkoani Geita.

Sauti ya Askofu Mondeha Kabeho

Nabii kiongozi wa kanisa la mlima wa moto katoro Meshack mpanduji akizungumza na Storm FM. Picha na Nickolaus Lyankando

Kwa upande wake Nabii kiongozi wa kanisa la mlima wa moto katoro Meshack mpanduji amewaomba watanzania kuacha kubeza shughuli zinazofanywa na serikali nabadala yake waiunge mkono  kwa kazi inayofanya.

Sauti ya Nabii Meshack Mpanduji
Nao baadhi ya manabii kutoka madhehebu Mbalimbali hapa nchini waliohudhuria katika kongamano hilo pamoja na waumini wameahidi kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita katika mapambano dhidi ya maadui wa taifa.

Sauti ya baadhi ya waumini na Manabii

Waumini wa kanisa la mlima wa moto Katoro wakiwa katika kongamano la kuliombea taifa. Picha na Nickolaus Lyankando

Kongamano hilo la Maombi limewakuatanisha zaidi ya manabii 18 wa makanisa ya PCMA kutoka hapa nchini.