

20 May 2025, 4:36 pm
Baadhi ya wananchi katika manispaa ya Geita wameshindwa kupata vyeti vya kuzaliwa kwa wakati kutokana na changamoto ya kusuasua kwa mtandao iliyopelekea kusubiri vyeti kwa zaidi ya saa nne ili viweze kuchapishwa.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya wananchi waliokuwa katika ofisi ya msajili vifo na vizazi wilaya ya Geita Mei 19, 2025 ambapo wamesema kusuasua kwa mtandao kumechangaia shughuli zingine kutofanyika huku wakiomba maboresho kufanyika ili kuondoa changamoto hiyo.
Afisa msajili msaidizi wilaya ya Geita ambaye pia ni Mratibu wa vizazi na vifo mkoa wa Geita Bi. Mwanne Abdallah amekiri kuwepo kwa changamoto ya kusuasua kwa mtandao ambao huwawezesha kuchapisha vyeti kwa haraka na kwamba inaathiri utendaji kazi na kusababisha msongano kwa wananchi wakati wa kupata huduma.
Sanjari na hayo amewasihi wananchi kuwa watulivu pindi inapotokea changamoto ya mtandao.