Storm FM

Wakazi wa Mwanza wamejitokeza kwa wingi kumuaga Dkt Magufuli

24 March 2021, 10:12 pm

Wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo ya mikoa jirani ya Shinyanga,Simiyu na Tabora wamejitokeza kwa wingi katika Uwanja wa CCM Kirumba kumuaga Dkt John Pombe Magufuli aliekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliefariki dunia Machi 17-2021 kwa tatizo la Moyo.

Baadhi ya watu waliojitokeza katika zoezi la kumuaga kiongozi huyo Joshua Obed na Yusta Ibangwa wamesema wamesikitishwa na kifo cha kiongozi huyo ambae alijipambanua kwa kuwatetea watu wanyonge ambao walikuwa wamekosa mtetezi.

Baada ya Mwili wa Dkt Magufuli kuagwa katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza ulielekea Mkoani Geita wilayani Chato kwa ajili ya shughuli za Maziko ambapo siku ya terehe 25 wakazi wa Mkoa huo na mikoa jirani watapata fursa ya kumuaga huku tarehe 26  itakuwa siku ya maziko.