Storm FM

Wafanyabiashara kupatiwa mikopo ya bei nafuu

26 November 2023, 12:54 am

Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi. Picha na Storm FM

Kilio cha wafanyabiashara kupata mikopo kutoka benki na kutambulika kibiashara, sasa imepata ufumbuzi baada ya wao wenyewe kusimama kidete kutetea hilo.

Na Daniel Magwina- Geita

Viongozi Chemba ya wafanyabiashara mkoa wa Geita wameanza ziara ya kutembelea Taasisi za fedha mkoa wa Geita kwa lengo la kuwatafutia frusa ya mikopo nafuu wafanyabiashara wadogo.

Akizungumza na Storm Fm Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi walipotembelea kwenye Benki za NBC pamoja na CRDB amesema kipaumbele chao ni kuhakikisha kila mfanyabiashara anapata mkopo wenye masharti nafuu ili kukuza Biashara zao.

Aidha kwa upande wa Meneja wa benki ya NBC Hilda Bwimbo na Meneja wa CRDB benki Erick Mayala wamesema wapo tayari kushirikiana na TCCIA Mkoa wa Geita ili kuzidi kutoa Elimu ya fedha kwa wafanyabiashara.

TCCIA Mkoa wa Geita wanatarajia kufanya Kongamano la wafanyabiashara wadogo mwishoni mwa mwaka huu ili kuwaonesha fursa za kibiashara ili kukuza uchumi wa mkoa wa Geita.