Storm FM

Alietaka kujinyonga afikishwa ofisi ya mtaa

3 April 2024, 2:42 pm

Hawa ni baadhi ya wananchi wakiwa katika ofisi ya mtaa wakishuhudia kufikishwa ofisini hapo kwa mwanamke alietaka kujinyonga. Picha na Kale Chongela

Matukio ya watu kujichukulia sheria mkononi yanaendelea kujitokeza katika maeneo mbalimbali kwasasa imefikia hatua ya baadhi ya watu kutaka kujitoa uhai kwasababu ambazo zinaweza kupata majibu.

Na Kale Chongela – Geita

Mwanamke Rejina Jumanne Mkazi wa mtaa wa Mpomvu kata ya Mtakuja Mjini Geita Mwenye umri wa miaka 28 amezua taharuki mara baada ya kufanya jaribio la kujiua lakini wasamalia wema walifika na kumkuta akifanya kitendo hicho na kumuokoa.

Akizungumza na Storm Fm Bi Rejina akiwa ofisi ya mtaa huo amesema alichukua maamuzi hayo ya yeye kujinyonga kutokana na mzozo baina yake na mama yake mzazi ambaye ametambulika kwa jina la Chausiku John kuwa mama yake mzazi amekuwa haonesha upendo juu yake

Sauti ya Mhanga wa tukio la kujinyonga

Baadhi ya majirani wamesema Rejina aliacha mtoto wake na kwenda pembezoni mwa nyumba ambayo alikuwa akiishi ndipo baadhi ya wasamalia wakalazimika kufuatilia ndipo wakabaini kuwa anataka kujinyonga na wakatoa taarifa kwa viongozi wa eneo hilo .

Sauti ya majirani na ndugu
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Bw Mathias Metusela amekiri mwanamke huyo kufikishwa ofisini kwake ambapo amebainisha kuwa kwa kushirikiana na wazee wa mtaa huo wametatua mgogoro huo kwa kuwasuluhisha wote kwa pamoja.

Sauti ya serikali ya mtaa

Hao ni baadhi ya wananchi wakiwa katika ofisi za mtaa wakishuhudia kufikishwa ofisini hapo kwa mwanamke alietaka kujinyonga. Picha na Kale Chongela