Storm FM

Waokolewa wakiwa hai baada ya kukaa chini ya ardhi kwa siku tisa

14 August 2023, 5:12 pm

Wananchi na mitambo iliyotumika kuwaokoa wachimbai wawili waliyofukiwa na kifusi. Picha na Mrisho Sadick

Matukio ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kufariki dunia katika Mkoa wa Geita yameendelea kujitokeza mara kwa mara huku sababu ya matukio hayo ikiwa ni uduni wa vifaa wanavyotumia.

Na Mrisho Sadick:

Wachimbaji wadogo wawili Mpina Shukuru (29) mkazi wa Mganza, wilayani Chato na Renatus Nyanga (35), mkazi wa Sengerema mkoani Mwanza, wameokolewa wakiwa hai, baada ya kufukiwa na kifusi siku tisa, katika mgodi wa Igalula; wilayani Nyangwale, Mkoa wa Geita.

Wachimbaji hao walifukiwa na kifusi usiku wa Agosti mosi, 2023; wameokolewa Agosti 11 huku wakiwa wamedhoofika na kupatiwa huduma ya kwanza na madaktari waliokuwa eneo la tukio, kisha kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nyang’hwale kwa matibabu zaidi.

Sauti ya wachimbaji waliyookolewa

Mganga Mfawidhi wa hiyo, Princepius Mugishagwe, amesema siku ya alhamisi Agosti 10, 2023 saa 2:30 usiku, walipokea taarifa ya wachimbaji kufukiwa na kifusi, ambapo timu ya dharura ya hospitali hiyo, ilifika kutoa msaada ambapo tayari walikuwa wametolewa kwenye kifusi.
Amesema afya zao zinaendelea vizuri na kwamba wanaweza kuruhusiwa muda wowote baada ya afya zao kutengemaa.

Sauti ya Mganga Mfawidhi