Storm FM

BRELA yaendelea kutoa elimu ya urasimishaji kwenye maonesho Geita

22 September 2023, 1:09 pm

Kaimu mkurugenzi wa kurugenzi ya miliki ubunifu kutoka wakala wa usajiri wa biashara na leseni BRELA, Roi Mhando. Picha na Zubeda Handrish

BRELA wanaendelea kuwa msaada mkubwa katika kutoa elimu ya urasimishaji wa biashara kwani imekuwa changamoto kubwa kwa wafanyabiashara.

Na Zubeda Handrish- Geita

Elimu na uelewa mdogo kuhusu urasimishaji wa biashara imekuwa changamoto kubwa kwa wafanyabiashara hali iliyowasukuma wakala wa leseni na biashara BRELA kuweka banda katika maonesho ya 6 ya teknolojia ya madini ili kutoa elimu hiyo.

Elimu kutoka BRELA ikiendelea katika viwanja vya EPZA maonesho, Geita. Picha na Zubeda Handrish

Hayo yamesemwa na kaimu mkurugenzi wa kurugenzi ya miliki ubunifu kutoka wakala wa usajiri wa biashara na leseni BRELA Roi Mhando wakati akiongea na waandishi wa habari wa mkoa wa Geita katika maonesho ya madini yanayotajaiwa kufunguliwa rasmi mnamo June 23.

Sauti ya kaimu mkurugenzi wa kurugenzi ya miliki ubunifu kutoka wakala wa usajiri wa biashara na leseni BRELA, Roi Mhando

Roi aliwasihi wafanyabiashara kufika mapema katika banda la brela ili kujipatia elimu bure na kufanya usajiri wa papo hapo ili kila mfanyabiashara aweye kuwa katika mfumo rasmi.

Aidha Roi aliongeza kuwa wamepokea maelekezo kutoka kwa naibu waziri wa viwanda na biashara mh Exaud Kigahe ya kuhakikisha wanawawezesha wafanyabiashara badala ya kuwa kikwazo kwao katika utoaji wa huduma.