Storm FM

Maonesho ya nne yanoga.

17 September 2021, 2:20 pm

Na Ester Mabula:

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imewataka wachimbaji kutumia Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini kujifunza teknolojia mbalimbali zilizopo kwenye maonesho  yaliyoanza leo Mkoani Geita.

Wito huo umetolewa leo Septemba 16, 2021 na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Seif Gulamali alipotembelea banda la Wizara ya Madini na taasisi zake katika Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yaliyoanza leo Septemba 16, 2021 katika Uwanja wa Bombambili EPZ.