Storm FM

Mtoto wa miezi 7 atupwa kichakani Geita

21 April 2021, 11:48 am

Na Mrisho Sadick:

Mtoto mchanga anaekadiriwa kuwa na umri wa miezi (7) amekutwa ametupwa kwenye kichaka huku akiwa  amefariki katika Mtaa Mtaa wa Nyanza halmashauri ya mji wa Geita Mkoani Geita.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia tukio hilo wameiambia Storm FM kuwa huenda kuna mwanamke alietoa ujauzito nakwenda kumtupa mtoto huyo katika  vichaka vya uwanja wa ccm kalangalala mjini Geita.

Mashuhuda wa Tukio

Watetezi wa haki za binaadamu na wasaidizi wa msaada wa kisheria mjini Geita,  Geita Legal Aid Centre (GELAC) wamelaani kutokea kwa tukio hilo  nakuiomba jamii kuachana na vitendo hivyo nakumrudia mungu.

Afisa Ustawi wa halmashauri ya mji wa Geita  Bw Casbety Byabato amesema matukio ya watoto kutupwa yapo kidogo nakutoa wito kwa wananchi pindi wanapofikwa na changamoto za maisha wafike katika ofisi yake badala ya kujichukulia sheria.