Storm FM

Bodaboda atapeliwa pikipiki Msalala road mjini Geita

14 June 2024, 10:30 am

Egesho la bodaboda mtaa wa Msalala road halmashauri ya mji wa Geita. Picha na Amon Mwakalobo

Suala la umakini hutajwa kuwa jambo muhimu zaidi katika eneo la kazi/biashara nk ambapo baadhi ya watu wameendelea kutapeli mali za watu kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo udanganyifu na kuwaacha watapeliwa njia panda.

Na: Amon Mwakalobo – Geita

Mwendesha pikipiki ya biashara maarufu bodaboda kutoka mtaa wa Msalala road katika egesho la Msufini halmashauri ya mji wa Geita ajulikanae kwa jina la Method Israel ametapeliwa pikipiki yake na mtu asiyemfahamu.

Tukio hilo limetoka Juni 07, 2024 majira ya saa mbili usiku ambapo mwanaume huyo amesema tapeli huyo alienda sehemu yake ya kazi ambapo pia anajihusisha na kazi ya kunyoa nywele (salon) na kumuomba amuazime pikipiki kwa dakika chache alipompa akaondoka nayo moja kwa moja hadi sasa.

Sauti ya Method Israel

Baadhi ya wanachi wakiwemo majirani zake katika eneo lake la kazi wameelezea tukio hilo kwa nyakati tofauti tofauti.

Sauti ya wananchi

Mwenyekiti wa bodaboda egesho la Msufini amewashauri waendesha bodaboda kuwa makini na wateja wanaoenda kwenye maeneo yao ya kazi na kuwaazima pikipiki zao lazima wawe wanawafahamu vizuri

Sauti ya mwenyekiti wa bodaboda