Storm FM

Watoto wajengwe katika misingi ya imani

5 April 2024, 5:04 pm

Wanawake mjini Geita wakiwa kwenye futari ya kikundi cha wanawake na Samia Geita . Picha Mrisho Sadick

Mwezi mtukufu wa ramadhani umekuwa chachu ya kujenga jamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo amani ,umoja na mshikamano.

Na Mrisho Sadick – Geita

Wanawake Mkoani Geita wametakiwa kutumia kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani kuwajenga watoto wao katika misingi ya kiimani ili kuandaa kizazi chenye hofu ya Mungu.

Kauli hiyo imetolewa na kaimu shekhe Mkuu wa Mkoa wa Geita Mbaraka Mbaraka katika iftari ya wanawake na watoto wanaoishi katika Mazingira magumu iliyoandaliwa na Kikundi cha Wanawake na Samia mjini Geita ambapo amesema kiongozi bora ni yule aliyepata malezi bora namwenye hofu ya Mungu huku akisisitiza wananchi kuendelea kuwa na umoja.

Wanawake mjini Geita wakiwa kwenye futari ya kikundi cha wanawake na Samia Geita . Picha Mrisho Sadick
Sauti ya kaimu shekhe Mkuu Geita

Katibu wa itikadi uenezi na mafunzo wa CCM Mkoa wa Andrew Mnunke Geita amewataka viongozi wa dini na watanzania kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili awatumikie kwa misingi ya utawala bora.

Sauti ya mwenezi wa CCM Mkoa wa Geita
Viongozi wa dini kiislamu Geita wakiwa kwenye futari. Picha na Mrisho Sadick

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake na Samia Mkoani Geita Adelina Kabakama ameitaka jamii kuacha kubaguana nabadala yake wapendane.

Sauti ya kikundi cha wanawake na Samia Geita