Storm FM

Watumishi sekta binafsi waiangukia serikali Geita

2 May 2024, 10:47 am

Wafanyakazi wa GGML wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mbogwe. Picha na Mrisho Sadick

Kwakuwa serikali ndie msimamizi mkuu wa shughuli zote hapa nchini imetakiwa kufanya tathimini ya utendaji kazi wa sekta binafsi kwani zinadaiwa kukabiliwa na changamoto nyingi.

Na Mrisho Sadick – Geita

Wafanyakazi wa sekta binafsi na sekta zisizo rasmi Mkoani Geita wameiomba serikali kuongeza nguvu ya kutatua changamoto zinazowakabili kwakuwa waajiri wengi wamekuwa wakiendesha sekta hizo kwa maslahi yao binafsi.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Mkoa wa Geita Daud Mhagama katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi ambayo kimkoa yamefanyika katika wilaya ya Mbogwe huku akisema miongoni mwa changamoto katika sekta hizo ni malimbikizo ya mishahara  kutofuata viwango vipya vya kima cha mshahara nakutowasilisha michango yao kwenye mifuko ya Jamii.

Sauti ya mratibu wa TUCTA mkoa wa Geita
Mratibu wa TUCTA akiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mbogwe. Picha na Mrisho Sadick

Mbunge wa Jimbo la Mbogwe Nicodemus Maganga amesema bado watumishi wengi wanakabiliwa na Changamoto nyingi nakuahidi kuwasemea Bungeni huku Mkuu wa wilaya hiyo Sakina Mohamed akiipongeza serikali ya awamu sita kwa kuendelea kupunguza changamoto za wafanya kazi.

Sauti ya Mbunge Mbogwe
Sauti ya mkuu wa wilaya Mbogwe
Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela akiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mbogwe. Picha na Mrisho Sadick

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela akiwa kwenye maadhimisho hayo amekiri kuwepo kwa changamoto kadhaa katika sekta binafsi nakuahidi kuzifanyia kazi.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Geita

Maadhimisho haya kwa mwaka huu yamebebwa na kaulimbiu isemayo “Nyongeza ya mishahara ni msingi wa mafao bora na nikinga dhidi ya hali ngumu ya maisha”.