Storm FM

Miradi ya bilioni 5.6 yakutwa na mapungufu

10 August 2023, 6:18 pm

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Geita Leonidas Felix akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake. Picha na Mrisho Sadick

Vitendo vya rushwa vimeendelea kuwa na athari kubwa hadi kwenye miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kwa ajili ya wananchi.

Na Mrisho Sadick:

Miradi 12  yenye thamani ya shilingi Bilioni 5.6 imebainika  kuwa na Mapungufu  na viashiria vya rushwa   wakati wa utekelezaji wake mkoani Geita.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa  TAKUKURU Mkoa wa Geita Leonidas Felix  wakati  akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ya utekelezaji wa taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia April had juni  mwaka huu ambapo amesema  jumla ya miradi  33 yenye thamani  bilioni 16 .8 imefuatiliwa.

Sauti ya Mkuu wa TAKUKURU Geita

Aidha amesema  katika kipindi hicho cha April hadi Juni   mwaka huu tasisi hiyo imetoa elimu ya mapambano dhidi  ya Rushwa  kwa makundi mbalimbai  ili kuhamasisha  UMMA Kuendelea kushiriki  mapambano dhidi ya Rushwa   ambapo jumla ya kazi 31  za uelimishaji zimefanyika .

Hata hivyo ameongeza  kuwa   kero 168 ziliibuliwa  kupitia vikao  vya makundi hayo  na kati ya kero hizo  zimeanza kutatuliwa  ikiwemo kuwatafuta walengwa ili kujibu malalmiko hayo.