Storm FM

Wivu wa mapenzi wamponza, serikali ya mtaa yachukua hatua

28 April 2026, 7:41 am

Pombe ya kienyeji ambayo ilikutwa na kinyesi ndani yake katika mtaa wa Mkoani. Picha na Kale Chongela

Serikali ya mtaa wa Mkoani imemkamata mwanamke aliyedaiwa kujisaidia katika diaba lililokuwa na pombe ya kienyeji kwa kile kilichoelezwa ni wivu wa kimapenzi katika eneo la Lukilini  mtaa wa Mkoani kata ya kalangalala manispaa ya Geita.

Na: Kale Chongela

Ikumbukwe kuwa tuko hilo lilitokea April 02, 2026 katika mtaa huo  ambapo baada ya mwanamke huyo kutendo tukio hilo alitokemea kusikijulikana na baada ya kurejea amejikuta anatiwa nguvuni.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bw Salvatory Daniel akizungumza na Storm FM amethibitisha kukamatwa kwa mwanamke huyo ambaye jina lake limehifadhiwa na kwamba amefikishwa kituo cha polisi kwa hatua zaidi za kisheria.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa

Mmiliki wa klabu ya pombe za kienyeji Bi. Elizabeth Francisco amesema kiu yake ni kulipwa gharama za uharibifu uliofanyika kiasi cha shilingi laki 5.

Sauti ya Elizabeth Francisco

Hata hivyo mwanamke huyo ambaye ametuhumiwa kutenda kosa hilo amekana kutohusika na tukio hilo.

Sauti ya mtuhumiwa
Muonekano wa ofisi ya serikali ya mtaa wa Mkoani, kata ya Kalangalala. Picha na Kale Chongela