Storm FM

Shule ya msingi Nyakato yaongoza ufaulu kata ya Nyanguku

17 May 2026, 4:07 pm

Diwani wa kata ya Nyanguku Elias Ngole akizungumza wakati wa hafla ya pongezi. Picha na Ester Mabula

Jumla ya wanafunzi 55 walihitimu shuleni hapo ambapo wanafunzi 50 walifaulu na kujiunga na kidato cha kwanza na kupelekea kushika nafasi ya kwanza kwenye kata hiyo huku masomo yaliyofaulisha vizuri yakiwa ni Kiswahili, Sayansi  na Uraia na maadili.

Na: Ester Mabula

Uongozi wa kata ya Nyanguku Manispaa ya Geita umefanya hafla ya kuipongeza Shule ya msingi Nyakato kwa kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba  mwaka 2025.

Diwani wa kata hiyo ambaye pia ni Naibu Meya Manispaa ya Geita Mhe. Elias Ngole amesema hafla hiyo ni kiashiria cha kuongeza juhudi zaidi na motisha kwa shule nyingine ili zifanye vizuri zaidi huku akiwapongeza walimu wa shule ya Nyakato kwa hatua hiyo.

Sauti ya diwani mhe. Elias Ngole

Muwakilishi wa ofisi ya mkurugenzi Manispaa ya Geita Bi. Mariam John  amesemea matokeo hayo ni kielelezo cha uongozi mzuri wa kata hiyo na kuwapongeza walimu wote kwa kazi nzuri ya kuwafundisha wanafunzi.

Sauti ya muwakilishi ofisi ya mkurugenzi Bi. Mariam John
Afisa elimu kata ya Nyanguku Innocent Damas akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Picha na Ester Mabula

Akizungumza Afisa elimu kata ya Nyanguku Mwl. Innocent Damas na mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi Nyakato Charles Laurent wamesema mafanikio hayo yametokana na jitihada za makusudi na mikakati iliyowekwa na walimu ili kuongeza ufaulu.

Sauti ya afisa elimu na mwalimu mkuu msaidizi

Kata ya Nyanguku ina jumla ya shule tano za msingi ambazo ni shule ya msingi Sinamwendwa, shule ya msingi Nyanguku, shule ya msingi Nyakato, shule ya msingi Mwagimagi na shule ya msingi Kakonda.

Mwalimu mkuu msaidizi shule ya msingi Nyakato Charles Laurent akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Picha na Ester Mabula