Storm FM

Wajilinda kuzuia ndoa za utotoni

12 May 2021, 9:28 am

Na Mrisho Sadick:

Wakazi wa kijiji cha Igate kata ya Nzera halmashauri ya wilaya ya Geita mkoani Geita wameweka mikakati ya  kutokomeza vitendo vya baadhi ya wazazi wenye tabia ya kuozesha watoto wadogo badala ya kuwapeleka shule.

Wakizungumza na Storm FM  kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wamesema kuna baadhi ya wazazi ambao wanawatumia watoto wa kike kama  chanzo cha uchumi katika familia kitendo ambacho hakikubaliki.

Sanjari na hayo wamesema wamelazimika kutumia jeshi la jadi sungusungu kujilindi  kutokana na eneo hilo kuwa na muingoiliano mkubwa wa watu kutoka maeneo mbalimbali kwa ajiri ya ulanguzi wa zao la nanasi.

Diwani wa kata ia Nzera kilipo kijiji Igate Bw Zephania Milimo amesema vitendo hivyo vimepungua kwa kuwa ameendelea kuwachukulia hatua kali baadhi ya wazazi wanaobainika kufanya vitendo hivyo.

Diwani Nzera – Zephania Milimo