Storm FM

Makonda atua Chato, asema Rais Samia hana ubaguzi

10 November 2023, 3:59 pm

Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda. Picha na Mrisho Sadick

Akiwa kwenye mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Ziwa Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda , leo November 10, 2023 amefika wilayani Chato na kuzungumza na wananchi.

Na Mrisho Sadick- Geita

Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda amesema Serikali ya Chama Cha mapinduzi chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inafanya kazi bila ubaguzi wala makundi.

Sauti ya Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda

Makonda amesema hayo katika Kata ya Mganza Wilayani Chato Mkoani Geita wakati wa mapokezo yake akitokea Mkoani Kagera na atakuwa na ziara ya siku mbili Mkoani Geita.