Storm FM

Mbio za baiskeli kupamba tamasha la Chato utalii festival

16 November 2023, 2:17 pm

Baadhi ya washiriki wa mbio za Baiskeli wakiwa katika shindano la utangulizi kuelekea shindano rasmi novemba 26,2023. Picha na Mrisho Sadick

Chato imedhamiria kukuza uchumi wake kupitia utalii kwa kutangaza vivutio vilivyopo katika eneo hilo kupitia matamasha mbalimbali ikiwemo la Chato Utalii Festival.

Kuelekea katika tamasha la Chato Utalii Festival Novemba 26 mwaka huu , Mkuu wa wilaya ya Chato Deusdedit Katwale amesema mbio za Baiskel za mashabiki wa Simba na Yanga zitatumika kuenzi nakuendeleza utamaduni wa watu wa Kanda ya Ziwa.

Mkuu wa wilaya ya Chato akizungumza na wananchi wa Buseresere baada ya kumalizika kwa shindano la Mbio za Baiskeli. Picha na Mrisho Sadick

Katwale amesema hayo katika shindano la utangulizi la mbio za Baiskel kwa Mashabiki wa Simba na Yanga katika Kata ya Buseresere wilayani humo ikiwa ni sehemu ya maandalizi Kuelekea katika tamasha hilo Novemba 26 hadi Disemba tatu mwaka huu katika viwanja vya Magufuli mjini Chato.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Chato
Baadhi ya washiriki wa mbio za Baiskeli wakiwa katika shindano la utangulizi kuelekea shindano rasmi novemba 26,2023. Picha na Mrisho Sadick

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha waendesha Baiskeli Mkoa wa Geita Raphael Ngereja amesema katika shindano hilo la utangulizi wamepata washindi 10 kati ya 20 waliyoshiriki ambao watauwakilisha mkoa wa Geita katika mashindao ya Chato Utalii Festival ambapo kunatakuwa na washiriki wengine kutoka Mwanza na Simiyu.

Sauti ya Katibu Chama cha Baiskeli Mkoa wa Geita

Mbio hizo za Kilometa 34 zimeanzia Kata ya Buseresere hadi Kata ya Bwanga zilikuwa na washiriki 20 huku mshindi wa kwanza akiwa ni Onana Amos Shabiki wa Simba amesema ataendelea kufanya mazoezi zaidi ili kujiandaa na mashindano rasmi.

Sauti ya mshindi wa mbio za Baiskeli