Storm FM

Wakulima wilayani Chato walalamikia ubovu wa miundombinu ya barabara

25 March 2021, 3:01 pm

Wakulima wa kata za Kachwamba na Kasenga wilayani Chato mkoani Geita  wanalazimika kuuza dumu la mahindi kwa shilingi 3500 badala ya 8000  kutokana na miundombinu mibovu ya barabara ambayo haiwawezeshi kusafirisha bidhaa hiyo kwa uharaka.

Wakizungumza  na Storm Fm kwa nyakati tofauti baadhi ya wakulima hao wamesema  kuwa barabara itokayo Kasenga kuelekea chato mjini imeharibika vibaya hali  inayowalazimu wakulima  hao  kuuza bidhaa zao kwa bei ya chini nakuiomba serikali kupitia wakala wa barabara za mjini na vijijini Tarura wilayani humo  kufanya tathimini ya ukarabati wa eneo hilo kwa kuwa barabara hiyo ndiyo uti wa mgongo wa uchumi kwa wakulima wa vijiji hivyo.

Aidha Meneja wa wakala wa barabara za mijini na vijijini wilayani Chato  mhandisi Chacha Saguda akizungumza kwa njia ya simu  juu ya barabara hiyo amesema wamepanga kuanza kukarabati kilomita 10 za barabara katika eneo hilo muda wowote.