Storm FM

Watoa huduma afya ya kinywa na meno waja na mpango

20 August 2023, 9:58 pm

Mganga Mkuu wa mkoa wa Geita (RMO) Omari Sukari. Picha na Zubeda Handrish

Afya ya kinywa na meno ni muhimu katika maendeleo ya taifa, kwani bila ya afya njema hata utendaji hautawezekana.

Na Zubeda Handrish- Geita

Mganga Mkuu wa mkoa wa Geita (RMO) Omari Sukari amewataka wataalamu na watoa huduma katika kitengo cha Afya ya Kinywa na Meno kuzingatia misingi ya utoaji huduma kwa kuzingatia ustaarabu, heshima na utu ili kuwapatia wananchi huduma bora.

Nae Deograsia Mkapa (DMO) Bukombe ametoa rai ya kufanya kazi bila ya ubaguzi kwa wataalamu hao wa Kinywa na Meno huku akiahidi kutoa ushirikiano kwao, huku Esaery Nyandoto ambaye ni Kaimu (DMO) Geita DC akisisitiza ushirikiano.

Sauti ya wataalamu wa Afya ya Kinywa na Meno

Hayo yamezungumzwa kwenye kikao cha tathimini ya utoaji huduma ya Afya ya Kinywa na Meno kwa wataalamu wa huduma ya Afya ya Kinywa na Meno wilaya zote mkoani Geita, jana Agosti 18, 2023 kwenye ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Geita.