Storm FM

Storm FM yazindua kipindi kipya cha Afya Chikobe

16 September 2023, 11:20 pm

Wanyakazi wa Storm FM katika uzinduzi wa kipindi kipya cha Afya cha Sauti Ya Tiba katika kijiji cha Chikobe. Picha na Zubeda Handrish

Katika kuelekea miaka 9 ya uwepo wa Kituo cha redio cha Storm FM mkoani Geita, tunayo furaha kukufahamisha juu ya uwepo wa kipindi kipya cha “Sauti Ya Tiba” ambacho kitajikita katika kutoa elimu na taarifa sahihi juu ya magonjwa mbalimbali.

Na Zubeda Handrish- Geita

Leo timu ya Storm FM ilifika katika kijiji cha Chikobe kata ya Nyachiluluma kwaajili ya kuzindua kipindi hicho ambapo sambamba na uzinduzi kulikuwa na burudani mbalimbali ikiwemo mpira wa Miguu ukiwakutanisha Chikobe Star vs Red Power ambao umekamilika kwa Chikobe Star kuibuka washindi kwa mikwaju ya penati 4-2.

Wananchi wa kijiji cha Chikobe, kata ya Nyachiluluma mkoani Geita. Picha na Zubeda Handrish

Kipindi cha Sauti ya Tiba kitasikika kila Ijumaa kuanzia saa 12 jioni hadi saa 12:30 jioni kwa udhamini wa Taasisi ya @esrftz kwa kushirikiana na Wataalam kutoka NIMR na Wataalam wa Afya kutoka Mkoani Geita.