Storm FM

Uwanja wa Magogo mbioni kukamilika

17 December 2022, 2:29 pm

Na Zubeda Handrish:

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Zahara Michuzi ametoa tathimini ya maendeleo ya uwanja utakaotumiwa na klabu ya @geitagoldfc ulioko Magogo akisema zaidi ya Bilioni 1.8 zimetumika hadi sasa huku bajeti ya awamu ya kwanza ya kukamilisha uwanja huo ikiwa ni Bilioni 2.4 huku akisema ni asilimia 90 ya uwanja huo imekamilika hadi sasa.

Nae kocha mkuu wa klabu hiyo Fred Felix Minziro amesema kikosi kinaendelea vizuri kwaajili ya michezo ya mkondo wa pili huku akidokeza wapo watakaoondoka na watakaobaki kikosini hapo katika dirisha hili dogo la usajili lililofunguliwa rasmi Dec 15, 2022.