Storm FM

Popo wavamia mtaa, wananchi wakumbwa na taharuki Geita

15 October 2023, 6:59 am

Changamoto ya popo katika baadhi ya maeneo Tanzania imeonekana kuwa ni sugu, hilo pia limetokea katika mtaa wa katikati ya mji wa Geita.

Na Zubeda Handrish- Geita

Wananchi wa mtaa wa Nyerere Road uliopo kata ya Kalangalala, halmshauri ya Mji wa Geita wamezungumzia kero ya popo inayowakabili bila ya kujua popo hao wametokea wapi na kurandaranda kwenye miti na makazi ya watu mtaani hapo.

Sauti ya wananchi wa mtaa wa nyerere Road uliopo kata ya Kalangalala, halmshauri ya Mji wa Geita

Naye kamanda wa Polisi Jamii katika mtaa huo wa Nyerere Road Patrick Paul amekiri kushuhudia popo hao na namna walivyoleta taharuki mtaani hapo, takribani wiki sasa tangu kadhia hiyo imeanza.

Sauti ya kamanda wa Polisi Jamii katika mtaa wa Nyerere Road, Patrick Paul

Nae Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa huo wa Nyerere Road amekiri kuwepo kwa Popo hao na kuwataka wananchi kuwa watulivu wakati wanaangalia namna ya kufanya kudhibiti hali hiyo.

Sauti ya Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Nyerere Road