Storm FM

Storm FM yampongeza mwandishi wake kushinda tuzo za EJAT

12 August 2023, 7:44 pm

Baadhi ya wafanyakazi na Mkurugenzi wa Storm FM wakiwa katika hafla ya kumpongeza mwandishi mwenzao Said Sindo. Picha na Ester Mabula

Mkurugenzi wa Kituo cha Redio cha Storm FM ameahidi kuendelea kutoa motisha kwa wafanyakazi wake wanaofanya vizuri katika nyanja mbalimbali ikiwemo tuzo.

Na Mrisho Sadick:

Storm FM imempongeza Mtangazaji na mwandishi wake Said Sindo kwa kushinda tuzo za umahiri za uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) kipengele Cha Haki za binadamu kwa upande wa Redio.

Hafla hiyo ya kumpongeza imefanyika katika viwanja vya Disire Park mjini Geita na zoezi hilo limeongozwa na Mkurugenzi wa Storm FM Modesta Mselewa na baadhi ya wafanyakazi wa 88.9 Storm FM.

Tuzo hizo zilitolewa Julai 22,2023 Mlimani City Jijini Dar es salaam na Sindo aliandaa Makala fupi inayoelezea changamoto ya mauaji ya walinzi yaliyokithiri Mkoani Geita na hatua zinazochukuliwa na serikali pamoja na wadau kukomesha vitendo hivyo nakuibuka mshindi.

Baadhi ya wafanyakazi na Mkurugenzi wa Storm FM wakiwa katika hafla ya kumpongeza mwandishi mwenzao Said Sindo. Picha na Ester Mabula