Storm FM

Viongozi wa dini Geita waipongeza serikali kuvutia wawekezaji

25 July 2023, 5:46 pm

Waumini wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste Geita CPCT wakishuhudia usimikwaji wa viongozi wa umoja huo wilaya ya Geita . Picha na Mrisho Sadick

Kutokana na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji hali ambayo imekuwa kivutio kikubwa cha wawekezaji jambo hilo limepongezwa na viongozi wa dini.

Na Mrisho Sadick:

Viongozi wa dini mkoani Geita wameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuvutia wawekezaji pamoja na kusogeza huduma muhimu kwa wananchi ikiwemo nishati ya umeme , maji , barabara na ujenzi wa vituo vya afya.

Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa umoja wa makanisa ya kipentekoste mkoa wa Geita (CPCT) Askofu Joshua William katika zoezi la kuwasimika viongozi wa umoja huo wilaya ya Geita kanisa la FPCT Geita mjini ambapo ameahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika shughuli mbalimbali za kuwaletea wananchi maendeleo.

Sauti ya Askof Joshua William
Askofu Joshua William Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste Geita CPCT . Picha na Mrisho Sadick

Mwenyekiti  wa CPCT wilaya ya Geita aliyesimikwa James Mjogo na mwenyekiti wa umoja huo kitengo cha wanawake Mkoa wa Geita Magdalena Masunga wamesema jukumu la kukemea mmomonyoko wa maadili nakujiletea maendeleo nilakila mmoja.

Sauti ya James Mjogo na Magdalena Masunga

Afisa tarafa wa Geita Cosmas Joseph akizungumza Kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Geita amesema serikali inatambua mchango wa viongozi wa dini huku akiwataka kuendelea kuongeza nguvu ili kukabiliana na vitendo viovu katika jamii ikiwemo uhalifu.

Sauti ya mwakilishi wa Mkuu wa wilaya