Storm FM

Idara ya mazingira Geita yaja na mikakati ya kudhibiti taka

1 September 2023, 4:25 pm

Vifaa maalum vya kutunzia taka vilivyowekwa na Idara ya Mazingira Geita. Picha na Kale Chongela

Uchafuzi wa mazingira na utupaji taka hovyo katika halmashauri ya mji wa Geita ambapo ndio kitovu cha mkoa, umepelekea idara ya mazingira kuja na mpango mkakati kudhibiti uchafuzi huo.

Na Kale Chongela- Geita

Idara ya Mazingira halmashauri ya mji wa Geita imekuja na mikakati ya kuweka vifaa maalum vya kutunzia taka ikiwa lengo ni kuhakikisha mji unakuwa katika hali ya usafi.

Akizungumza na Storm FM  Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira Mjini  Geita  Bw. Aloyce Mtayuga amesema vifaa hivyo vimewekwa pembezoni mwa barabara ikiwa ni kuhakikisha, wananchi hawapati usumbufu wa wao kutunza taka ambazo wanajizalisha.

Sauti ya Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira Mjini  Geita  Bw. Aloyce Mtayuga

Aidha Bw. Mtayuga ameongeza kwa kusema licha ya uwepo wa vifaa hivyo maalumu kwa ajili ya kutunzia taka, yapo pia magari ambayo ni maalumu kwa ajili ya kubeba taka  hizo.