Storm FM

Mtoto azaliwa bila mikono

23 April 2021, 6:37 pm

Na Joel Maduka:

Baraka Marko mkazi wa Nemba Wilaya ya Biharamulo amewaomba watanzania wenye mapenzi mema kumsaidia kupata baiskeli  ndogo ya magurudumu matatu ambayo itamsaidia mtoto wake ambaye anaitwa Faraja Baraka aliyemzaa bila ya kuwa na mikono kutokana na sasa amekuwa akipata wakati mgumu wa kumuhudumia kutokana na kukosa kifaa cha kumbebea.

Akizungumza na Storm FM   mjini Geita Bw Baraka amesema  tatizo la mtoto huyo  alizaliwa akiwa anaviungo vya mikono na kwamba amekuwa akipitia wakati mgumu kwenye malezi yake kutokana na  wakati mwingi wamekuwa ni mtu wa kumuhudumia kutokana na hali aliyonayo.

Baraka anadai kwa sasa anawatoto wawili na binti yake mwenye ulemavu wa mikono ni wa kwanza ana umri wa miaka mitatu na wa pili anamiezi minne na kwamba  kutokana na hali ya mtoto wake baadhi ya majirani wamekuwa na minongo’no ya kuona kama kuna jambo la tofauti lilitendeka wakakti wa kumzaa mtoto huyo.

Kwa mtu ambaye ataguswa na taarifa hii unaweza kuwasiliana na Baraka kwa Namba 0756235651