Storm FM

Kumzuia mtu kufanya majukumu yake ni kosa kisheria

7 July 2023, 12:12 pm

Kupitia Pekuzi za Mtaa kwa Mtaa (Storm Asubuhi) iliruka taarifa ya mkakanganyiko wa mabadiliko ya uongozi uliotokea kati ya Diwani wa kata ya Tabaruka Sospeter Busumabu na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Sengerema Binuru Shekhidele kutaka kubadili uongozi nafasi ya afisa mtendaji baada ya afisa mtendaji wa kijiji cha Busulwangili Jonesia Ntalala kukataliwa na wananchi, na Diwani Busumabu kwa kushirikiana na wananchi kumuweka madarakani afisa maendeleo wakati Mkurugenzi yeye akimpatia majukumu afisa mtendani mpya kuchukua nafasi hiyo.

Wakili wa serikali mkoa wa Geita Maganga Dominick. Picha na Zubeda Handrish

Muingiliano wa majukumu katika baadhi ya sekta ziwe za serikali au binafsi umekithiri kiasi cha amani kukosekana na kusababisha migogoro katika maeneo ya kazi, hili limepelekea kumtafuta wakili wa serikali mkoa wa Geita Maganga Dominick ili kutolea ufafanuzi.

Na Zubeda Handrish- Geita

Taarifa hiyo ilionesha mgongano wa kimajukumu ikimuonesha Diwani Busumabu akihoji sababu zilizopelekea Mkurugenzi Binuru kumpa majukumu mtu mwingine wakati yeye na wananchi wameshamchagua kiongozi mpya, hilo limepelekea kumtafuta wakili wa serikali Maganga Dominick kutolea ufafanuzi wa kisheria juu ya mipaka yakiutendaji akianza na uelewa wa kawaida pamoja na majukumu ya afisa mtendaji.

Sauti ya wakili wa serikali mkoa wa Geita Maganga Dominick akitolea ufafanuzi wa kisheria juu ya mipaka ya kiutendaji

Lakini pia Wakili Maganga amefafanua pia majukumu ya Diwani na mipaka yake ya kazi.

Sauti ya wakili wa serikali mkoa wa Geita Maganga Dominick akitolea ufafanuzi wa kisheria juu ya mipaka ya kiutendaji