Storm FM

Duka laungua moto.

3 August 2021, 1:54 pm

Na Zubeda Handrish:

Duka la vyombo la vyumba viwili limeungua moto katika mtaa wa Mission uliopo katika halmashauri ya mji wa Geita huku chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijafahamika.

Mmiliki wa duka hilo Bw. Venas John Mpalamawe amesikitishwa na tukio hilo na kuwashukuru raia wema kwa kuwahi kutoa taarifa kwa wakati kwa Jeshi la zimamoto na uokoaji ambapo waliwahi kudhibiti moto huo kabla ya kuteketeza duka lote na kuleta madhara zaidi.

Nao baadhi ya majirani waliokuwa katika tukio wamezungumzia namna walivyoshtushwa na tukio hilo kutokana na madhara yaliojitokeza katika duka hilo.

Aidha Kamishna Msaidizi Mwandamizi Kamanda wa jeshi la zima moto na uokoaji mkoa wa Geita Zabron Muhumha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwaasa wamiliki wa maduka kuhakikisha wanakua na vifaa vya tahadhari dhidi ya majanga ya moto na walinzi kuwa waaminifu katika kazi zao.