Storm FM

Geita kuendelea kuwaenzi mashujaa kwa vitendo

25 July 2023, 5:26 pm

Mnara wa Mashujaa mkoani Geita . Picha na Mrisho Sadick

Wananchi na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Geita wamejitokeza katika viwanja vya Mashujaa kuadhimisha kumbukumbu ya mashujaa waliojitoa maisha yao kwa ajili ya watanzania.

Na Mrisho Sadick:

Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe Martin Shigela amesema mkoa wa Geita utaendelea kuwaenzi kwa vitendo mashujaa wote waliojitoa maisha yao kulipigania taifa.

Mhe Shigela ametoa kauli hiyo katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa katika viwanja vya Mashujaa mjini Geita ambapo amesema mkoa wa Geita utaendelea kuwaenzi mashujaa wote waliopigana kwa ajili ya taifa.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Geita
Mkuu wa Mkoa wa Geita watano kutoka kushoto akiwa na viongozi mbalimbali katika kumbukumbu ya mashujaa . Picha na Mrisho Sadick

Kwa upande wake Sajenti Mstaafu wa Jeshi la Polisi aliyepigana vita vya Kagera ameiomba serikali kuendelea kuwakumbuka mashujaa wote kwa kuwa walijitoa kwa ajili ya watanzania wote.

Sauti ya Sajenti Mstaafu