Storm FM

Storm FM yafungua mwaka 2022 na Bonanza la michezo.

3 January 2022, 10:42 am

Na Zubeda Handrish:

Kituo cha redio cha Storm FM kimeanza mwaka mpya wa 2022 kwa Bonanza la Michezo mbalimbali ikiwemo kukimbiza kuku, Mpira wa miguu, Kukimbia na yai kwenye kijiko ambalo na mingineyo, lililofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Uwanja kata ya Nyankumbu mjini Geita, huku timu ya Storm FM ikiingia mtaani kuzungumza na wakazi wa mtaa huo.

Washindi wa Michezo mbalimbali katika Bonanza la kuukaribisha Mwaka Mpya walikabidhiwa zawadi zao kutoka kwa wadhamini ambao ni Storm FM,  SML na Mcharo Entertainment katika Dimba la Shule ya Msingi Uwanja.