Storm FM

Mgogoro wakulima na wafugaji waitesa Chikobe

19 September 2023, 10:44 pm

Mkazi wa kijiji cha Chikobe. Picha na Said Sindo

Changamoto ya wakulima na wafugaji bado imeendelea kusumbua katika baadhi ya maeneo mkoani Geita.

Na Said Sindo- Geita

Wakulima wa kijiji cha Chikobe kata ya Nyachiluluma, wilayani na mkoani Geita wamesema wapo hatarini kukumbwa na njaa baada ya mashamba yao kuharibiwa na mifugo ya wakulima ambao wamekuwa wakilisha mifugo katika mashamba yao.

Wakizungumza na Storm Fm kijijini hapo, wakulima hao wamesema imekuwa ni kero na kikwazo cha maendeleo kwa wakulima huku wanapojaribu kuiondoa, wakitishiwa kufanyiwa vitendo vya kinyama ikiwemo kupigwa.

Sauti ya wakulima kijiji cah Chikobe
Sauti ya wakulima kijiji cah Chikobe
Mkazi wa kijiji cha Chikobe. Picha na Said Sindo

Mtendaji wa kata ya Nyachiluluma Emmanuel Shabani Itanaki amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo huku akisema kesi za wafugaji kuingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima zimeshatafutiwa ufumbuzi ikiwemo kutungwa sheria ndogo za kutoza faini kwa watakaokamatwa.

Sauti ya Mtendaji wa kata ya Nyachiluluma Emmanuel Shabani