Storm FM

Kijana akamatwa usiku wa manane akidaiwa kuiba debe mbili za mpunga

7 September 2023, 7:57 pm

Kijana aliyedaiwa kuiba debe mbili za mpunga. Picha na Nicolaus Lyankando

Matukio ya wizi katika maeneo mbalimbali mkoani Geita yanaendelea kujitokeza licha ya jitihada ya Jeshi la Polisi mkoa wa Geita kwa kushirikiana na Jeshi la Jadi.

Na Nicolaus Lyankando- Geita

Kijana mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 27 amekamatwa usiku wa manane akidaiwa kuiba debe mbili za mpunga katika kitongoji cha Mjimwema, kijiji cha Lulembela, wilayani Mbogwe, mkoani Geita.

Wakizungumzia kukamatwa kwa kijana huyo baadhi ya wananchi walioshiriki katika doria usiku huo wamesema walimkamata akiwa anakokota baskeli akiwa amebeba debe mbili za mpunga lakini baada ya kumhoji alidai yeye ni mfanyabiashara anapeleka sokoni mpunga huo.

Sauti ya wananchi walioshuhudia tukio

Kwa upande wake kijana anaedaiwa kuiba mpunga aliejitambulisha kwa jina la Oseph Masanja amekana tuhuma hizo.

Sauti ya kijana anaedaiwa kuiba debe mbili za mpunga
Kijana aliyedaiwa kuiba debe mbili za mpunga. Picha na Nicolaus Lyankando

Moja mwananchi katika eneo hilo amesema kwa sasa matukio ya vibaka yamemurudisha nyuma kimaendeleo baada ya kuibiwa mara mbili ndani ya siku 30.

Sauti ya moja mwananchi katika eneo hilo

Akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa eneo hilo ambae pia ni mtemi wa jeshi la sungu sungu Enock Bujashi ametoa rai kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo na polisi ili kutokomeza matukio hayo.

Sauti ya Enock Bujashi akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa eneo

Lakini pia akatoa rai kwa vijana kuendelea kufanya kazi za halali na si kuiba, kwani taifa bado linawategemea katika kuinua pato la nchi kwa ujumla.