Storm FM

Afisa Mtendaji Ibolelo Atoweka Na Zaidi Ya Laki 800,000 Za Wananchi

19 May 2021, 7:20 pm

Na Kale Chongela:

Wakazi wa Mtaa wa Ibolelo kata ya Nyankumbu  Halmashauri ya mji wa Geita  wamewaomba viongozi wa eneo hilo kumfuatilia na kurejesha kiasi cha Fedha   shilingi Laki nane Tisini na Tatu Elfu iliyotumiwa na  aliyekuwa afisa mtendaji wa kijiji hicho anaedaiwa kutokomea kusikojulikana.

Wakizungumza kwenye Mkutano wa  hadhara   wenye lengo la kusoma mapato na matumizi  wananchi wa eno hilo wametumia fursa hiyo kudai pesa ambazo zilichukuliwa na aliyekuwa afisa Mtendaji wa Mtaa huo kuondoka na pesa ambazo zilichangwa na wananchi .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa huo Bw Stephano Magidinga amesema licha ya wananchi  kuonesha jiitihada za kuchagia michango mbalimbali  kwa ajiri ya ujenzi wa shughuli za mitaa   bado wapo baadhi ya watumishi ambao sio wadirifu .

Aidha afisa  Mtendaji wa Mtaa huo Bw Dionisi Lubihu amesema baada ya kuripoti katika ofisi hiyo alipewa malalamiko hayo na kuyafikisha kwa viongzi walioko juu yake  kuona namna ya kutatua changamoto hiyo