Storm FM

Moto wateketeza vitu vyote vya ndani Geita

13 July 2023, 12:27 pm

Jeshi la Zimamoto likipambana kuuzima moto uliyowaka katika chumba. Picha na Kale Chongela

Majanga ya moto mkoani Geita yameendelea kujitokeza huku wananchi wakitakiwa kutoa taarifa mapema kwa Jeshi la Zimamoto kwa ajili ya uokozi kwa namba ya bure ya 114.

Na Kale Chongela

Moto ambao haujajulikana chanzo chake umezuka na kuteketeza vitu vya ndani katika chumba kwenye nyumba iliyopo mtaa Mkoani kata ya Kalangalala katika Halmashauri ya Mji wa Geita Mkoani Geita nyakati za mchana.

Moto huo umetokea nyakati za saa sita mchana Jumatano ya Julai 12, 2023 ambapo baadhi ya wananchi waliungana na kuzima moto huo awali.

Mmiliki wa Nyumba hiyo Bi. Agnes Francis ameeleza kwa masikitiko tukio hilo namna lilivyotokea

Sauti ya Mmiliki wa Nyumba Bi Agnes Francis

Katika zoezi la kujinasua na tukio hilo, baadhi ya wananchi wa eneo hilo waliungana na kushiriki katika zoezi la kuuzima ili kuzuia athari zaidi.

Sauti ya shuhuda aliyezima moto

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji mkoani Geita Inspekta Edward Lukuba ametoa rai kwa wananchi kuwa waangalifu na pindi majanga yanapojitokeza watoe taarifa kwa Jeshi hilo kupitia namba ya bure ambayo ni 114.

Sauti ya Kaimu kamanda wa Jeshi la Zimamoto Mkoani Geita