Storm FM

Wanachama wa CCM Nyarugusu wachangia ujenzi wa ofisi ya chama.

4 January 2023, 8:30 am

Na Kale Chongela:

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Kata ya Nyarugusu wilayani Geita kwa kauli moja wameamua kuchangishana fedha kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya chama ya Kata itakayogharimu kiasi cha Shilingi Milioni ( 50 ) ili kurahisisha utolewaji wa huduma.


Wakizungumza na Storm FM katika eneo la ujenzi wa Ofisi hiyo baadhi ya wanachama wa Chama hicho wamesema Kata hiyo haina Ofisi rasmi ya Kata, ndio sababu iliyowasukuma kujitolea kuanzisha ujenzi wa Ofisi hiyo Kwa kauli moja.

Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa Evarist Gervas na Mjumbe wa Kamati ya siasa Mkoa wa Geita Renatus Sangano wakiwa katika zoezi la uchimbaji wa msingi wamesema katika kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt Samia Suluhu Hassan wamedhamiria kuweka Mazingira rafiki ya kufanyia kazi kwa viongozi wa Chama hicho.